Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Azam FC imesema inaendelea kufanya uchunguzi kuhusu hali ya kiafya iliyowakumba baadhi ya wachezaji wake baada ya kuripotiwa kupata maumivu ya tumbo na kichwa katika mazingira tofauti.
Taarifa zilizopo zinaeleza kuwa wachezaji saba wa kikosi hicho walionyesha dalili za kutokuwa sawa kiafya huku baadhi yao wakipelekwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi.
Haliyo ilitokea baada ya mchezo uluowakutanisha TRA united dhidi ya Azam kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha ambapo Azam walipikea kichapo Cha 4-1.
Hata hivyo, uongozi wa Azam FC umeeleza kuwa bado unaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha sintofahamu hiyo kabla ya kutoa taarifa rasmi yenye majibu ya kina kuhusu tukio hilo.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

.jpg)
Post a Comment