ARSENAL WATOA MKOSI BAADA YA MIAKA 22, WATWAA UBINGWA EPL 2025/26

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Imekuwa miaka 22 toka Arsenal wachukue ubingwa kwa aina ya kipekee, ubingwa wa kutofungwa maarufu kama The Invincibles, lakini baada ya safari ndefu ya maumivu, presha na mapambano makubwa, hatimaye wamerejea tena kileleni mwa soka la England kwa kutwaa taji la Premier League msimu wa 2025/26 chini ya kocha Mikel Arteta.

Arsenal wametwaa ubingwa huo wakiwa wamebakiza mchezo mmoja mkononi baada ya Manchester City kulazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Fc Bournemouth, matokeo yaliyowafanya mashabiki wa Arsenal waliokuwa nyumbani kuanza shangwe za ubingwa mapema kabla hata ya mchezo wao wa mwisho,hili ni taji lililokuja baada ya misimu mingi ya kusubiri huku wakishuhudia timu nyingine zikitawala England.

Mara ya mwisho Arsenal kutwaa ubingwa wa ligi ilikuwa msimu wa 2003/04 chini ya gwiji Arsene Wenger, msimu ambao waliandika historia kwa kutwaa ubingwa bila kupoteza mchezo hata mmoja. Kabla ya hapo walitwaa taji mwaka 1997/98, na sasa 2025/26 linaingia kwenye historia kama taji jingine kubwa kwa kizazi kipya cha Arsenal chini ya Arteta.

Moja ya siri kubwa ya mafanikio yao msimu huu ni uimara wa safu ya ulinzi, ambapo Arsenal wameruhusu mabao 26 pekee, idadi ndogo zaidi kwenye ligi hiyo. Mbali na ubora huo, pia wameonyesha nidhamu ya hali ya juu kwa kumaliza msimu bila kupata kadi nyekundu hata moja, jambo lililoonyesha ukomavu na umoja mkubwa ndani ya kikosi hicho.

0767915474,

lugembetimothy01@gmail.com




0/Post a Comment/Comments