Timothy Lugembe
Mwanakwetusports.
Klabu ya FC Barcelona imepata pigo kubwa baada ya kinda wake nyota Lamine Yamal kuthibitishwa kuwa nje ya uwanja kwa muda uliosalia wa msimu kutokana na jeraha la msuli wa nyuma ya paja (hamstring).
Yamal alipata majeraha hayo katika mchezo dhidi ya Celta Vigo, ambapo aliumia dakika ya 40 mara baada ya kupiga mkwaju wa penati uliowapa ushindi timu yake wa 1-0, tukio hilo lilimlazimu kinda huyo kuondolewa uwanjani, jambo lililoibua hofu kwa benchi la ufundi na mashabiki wa Barcelona.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa majeraha hayo ni makubwa kiasi cha kumuweka nje hadi mwisho wa msimu, hali inayopunguza nguvu ya safu ya ushambuliaji ya Barcelona katika kipindi kilicho salia kuelekea kumaliza msimu.
Hata hivyo, matumaini bado yapo kwa nyota huyo kurejea uwanjani kwa wakati kabla ya michuano ya FIFA World Cup, jambo ambalo linatoa faraja kwa mashabiki wa timu ya taifa ya Hispania.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment