YAMAL ATOA UJUMBE WA FARAJA KWA BARCELONA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kinda nyota wa klabu ya Fc Barcelona Lamine Yamal amewafariji mashabiki wa klabu yake kufuatia kuondoshwa katika robo fainali ya UEFA Champions League na Atletico Madrid.

Barcelona ilishindwa kufika hatua ya nusu fainali baada ya kupoteza katika mchezo mgumu uliokuwa na ushindani mkubwa, matokeo yaliyozima ndoto ya kutwaa taji hilo msimu huu.

Katika ujumbe wake kwa mashabiki, Yamal alieleza kuwa licha ya juhudi kubwa walizoweka, bado haikutosha kufanikisha malengo yao, akisisitiza kuwa hii ni sehemu ya safari ya mafanikio.

“Tulitoa kila kitu, lakini haikutosha, hii ni sehemu tu ya safari, kufika kileleni lazima upande, na haitakuwa rahisi,” alisema nyota huyo

Yamal aliwataka mashabiki kuendelea kuwa na imani na timu hiyo, akisisitiza kuwa kushindwa si mwisho bali ni funzo kwa mafanikio yajayo.

“Lakini kumbukeni kwamba kukata tamaa si chaguo, tuna sababu zaidi ya kutosha za kuamini, tutajifunza kutokana na kila kosa,” aliongeza.

Katika ujumbe wake huo, Yamal pia aliahidi kuwa Barcelona itarejea kwa nguvu zaidi na kupigania mafanikio makubwa siku zijazo.

“Sisi ni Barca, na tutarudi nafasi yetu, tutaleta Kombe la Mabingwa hapa,” alisisitiza.

Licha ya maumivu ya kutolewa, kauli hiyo ya Yamal imeonekana kuwapa matumaini mapya mashabiki wa Barcelona, wakiamini kuwa kizazi kipya cha wachezaji kinaweza kuirejesha klabu hiyo kwenye ubora wake barani Ulaya.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments