XAVI SIMONS ALIKOSA KOMBE LA DUNIA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kiungo mshambuliaji wa Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya Uholanzi, Xavi Simons, rasmi atakosa michuano ya kombe la Dunia baada ya kupata jeraha la goti.

Taarifa hiyo imekuja kama mshtuko mkubwa kwa mashabiki na benchi la ufundi, hasa ikizingatiwa mchango wake muhimu ndani ya kikosi Cha uholanzi, Simons alithibitisha hali hiyo kupitia ujumbe wake binafsi akieleza kuwa msimu wake umefikia mwisho ghafla huku akijikuta katika wakati mgumu wa kukabiliana na hali hiyo.

“Nimevunjika moyo, hakuna kinachoeleweka kwa sasa,” alinukuliwa akisema, akionesha maumivu ya kupoteza nafasi ya kuichezea nchi yake katika jukwaa kubwa la dunia.

Aidha, kiungo huyo alisisitiza kuwa ndoto yake kubwa ilikuwa kuipigania timu yake na kuiwakilisha nchi yake katika Kombe la Dunia, lakini sasa ndoto hiyo imelazimika kusubiri. Pamoja na maumivu hayo, ameahidi kurejea akiwa imara zaidi, akibainisha kuwa atapitia kipindi hiki kwa imani, uvumilivu na matumaini makubwa ya kurudi uwanjani.

Kwa upande mwingine, jeraha la Simons linaongeza orodha ya wachezaji nyota wanaokumbwa na majeraha kuelekea michuano hiyo ya dunia, hali inayozidi kuzua wasiwasi kwa timu mbalimbali kuhusu uimara wa vikosi vyao kabla ya kuanza kwa FIFA World Cup 2026.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments