Waamuzi wa Morocco kuchezesha Dabi ya Kariakoo Mei 3

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mchezo wa dabi ya Kariakoo kati ya Young Africans SC na Simba SC unaotarajiwa kuchezwa Mei 3, 2026 katika dimba la Meja Jenerali Isamuhyo, limechukua taswira mpya baada ya waamuzi wa mchezo huo kutoka nje ya nchi.

Hatua hiyo imekuja Katika kuhakikisha kunakuwa na uendeshaji bora wa mchezo huo, waamuzi kutoka Morocco wameteuliwa kusimamia pambano hilo, Mwamuzi wa kati atakuwa Hamza El Faruq, akisaidiwa na Lahsene Azkawi na Hamza El Nasri, huku Mostafa Kchaaf akichukua nafasi ya mwamuzi wa akiba.

Uamuzi wa kuwatumia waamuzi wa kigeni unaelezwa kulenga kuongeza uwazi na kuondoa malalamiko yanayojitokeza mara kwa mara kwenye michezo mikubwa ya ndani, Kwa uzoefu wao, waamuzi hao wanatarajiwa kuhakikisha mchezo unaendeshwa kwa haki na kufuata sheria zote za soka.

Kwa hali hiyo, matarajio ya wengi ni kuona dabi yenye ushindani mkali lakini yenye uamuzi wa haki, ambapo ubora wa timu uwanjani utaamua matokeo badala ya mjadala wa maamuzi ya waamuzi baada ya mchezo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com




0/Post a Comment/Comments