Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Nyota wa Brazil na klabu ya Real Madrid Vinicius Junior, ameweka wazi dhamira yake ya kuendelea kuitumikia klabu yake kwa muda mrefu baada ya kuthibitisha kuwa yuko tayari kusaini mkataba mpya.
Akizungumza kuhusu hatma yake, Vinicius alisema kuwa kwa wakati sahihi atafanya maamuzi ya kuongeza mkataba wake na kubaki ndani ya kikosi hicho kwa muda mrefu, akisisitiza kuwa Real Madrid ni klabu ya ndoto zake.
Mshambuliaji huyo alieleza kuwa bado ana mwaka mmoja uliosalia kwenye mkataba wake wa sasa, lakini hana presha yoyote kuhusu mazungumzo ya kuongeza mkataba, akionesha imani kubwa kwa rais wa klabu hiyo, Florentino Perez.
Aidha, Vinicius aligusia mahusiano yake mazuri na benchi la ufundi, akieleza kuwa ana uhusiano wa karibu na Alvaro Arbeloa kama alivyokuwa nao kwa Carlo Ancelotti, hali inayomsaidia kuelewa vyema majukumu yake uwanjani.
Kauli hiyo inaongeza matumaini kwa mashabiki wa Real Madrid kuwa nyota huyo ataendelea kuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya klabu hiyo kwa miaka ijayo.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment