Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Chelsea FC imeendelea kupitia kipindi kigumu katika English Premier League baada ya kupoteza michezo minne mfululizo huku ikishindwa kufunga bao hata moja.
Katika mfululizo huo mbaya, Chelsea ilianza kwa kupokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Newcastle United, na kufungwa 3-0 na Everton FC , 3-0 dhidi ya Man city na kipigo Cha 1-0 dhidi ya United hapo Jana na kukamilisha idadi ya vipigo vinne mfululizo bila bao.
Vipigo hivyo vinaifanya Chelsea kusalia nafasi ya sita wakiwa na alama 48 , mwenendo ambao unatia shaka kwa timu hiyo kufuzu mashindano ya UEFA champions league msimu ujao ambapo mpaka sasa EPL itapeleka timu tano na wao wapo nafasi ya sita ambapo kama msimamo utasalia hivyo watashiriki Europa league.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment