Sowah apelekwa Simba U-20 kama adhabu ya kinidhamu

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Simba SC imemrejesha kiungo wake, Sowah, katika kikosi cha vijana cha chini ya miaka 20 (U-20) kama sehemu ya adhabu kufuatia utovu wa nidhamu ulioripotiwa hivi karibuni.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, uongozi wa Simba umechukua uamuzi huo ili kumpa nafasi mchezaji huyo kujirekebisha, huku akianza mazoezi na kikosi hicho cha vijana chini ya uangalizi maalum wa benchi la ufundi, Hatua hiyo inalenga kumjenga upya katika misingi ya nidhamu, kujituma pamoja na kurejesha kiwango chake ndani ya klabu.

Inaelezwa kuwa Sowah atakuwa akifuatiliwa kwa karibu maendeleo yake katika mazoezi hayo, ambapo iwapo ataonyesha mabadiliko chanya ya tabia na kiuchezaji, ataweza kurejeshwa tena katika kikosi cha timu ya wakubwa kwa ajili ya michezo ijayo.

Uamuzi huo unaonekana kuwa sehemu ya msimamo wa Simba SC katika kuhakikisha nidhamu inazingatiwa kwa wachezaji wote, huku ukitoa ujumbe kwamba hakuna mchezaji aliye juu ya taratibu na maadili ya klabu.

0767815473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments