Timothy Lugembe
Mwanakwetusports.
Mchezaji Gianluca Prestiani amefungiwa michezo sita na UEFA kufuatia tukio lililomhusisha na Vinicius Junior ,adhabu hiyo imetolewa baada ya uchunguzi kubaini mwenendo usiofaa uliokiuka maadili ya mchezo.
Kwa mujibu wa UEFA, sehemu ya adhabu hiyo inatokana na matumizi ya lugha ya kejeli yenye mwelekeo wa ubaguzi (homophobic insults). Hata hivyo, imeelezwa wazi kuwa hakuna ushahidi wa maneno ya ubaguzi wa rangi katika tukio hilo.
Kutokana na uamuzi huo, Prestiani atakosa michezo sita ijayo, huku hatua hiyo ikiendelea kuibua mjadala kuhusu nidhamu ya wachezaji na umuhimu wa kuheshimu maadili katika soka la kimataifa.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment