Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Singida Black Stars imetangaza rasmi kuvunja benchi zima la ufundi kuanzia Aprili 5, 2026, ikiwa ni hatua ya haraka kufuatia mwenendo mbaya wa timu katika michezo ya hivi karibuni ya ligi kuu.
Uongozi wa klabu hiyo umeeleza kuwa maamuzi hayo yamechukuliwa baada ya timu kushindwa kupata matokeo ya kuridhisha ambapo hivi karibuni walikubali vichapo kutoka kwa Azam fc 2-1, na 2-0 dhidi ya TRA , hali iliyowalazimu kuchukua hatua za mabadiliko ili kurejesha ushindani.
Mbali na kuvunja benchi la ufundi, klabu hiyo pia imetangaza kupunguza mishahara ya wachezaji wote kwa asilimia 40 kuanzia April 6 2026 ,hadi mwisho wa msimu, hatua hiyo inaenda sambamba na kufuta bonasi zote zilizokuwa zikitolewa timu inaposhinda pamoja na kupunguza posho za safari kwa kiwango hicho hicho.
Uongozi wa klabu umeongeza kuwa utaendelea kutoa taarifa zaidi kuhusu benchi jipya la ufundi wakati wowote utakapokamilika mchakato wa kupata makocha wapya, huku ukisisitiza dhamira ya kurejesha timu kwenye kiwango Bora.
0767915474,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment