Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Simba SC imeshuka katika viwango vipya vya ubora wa vilabu barani Afrika vinavyotolewa na CAF, baada ya kuwa na msimu mbovu wa mashindano ya kimataifa 2025/26.
Kwa mujibu wa viwango hivyo, Simba imeshika nafasi ya 11 ikiwa na alama 38, ikishuka kutoka nafasi ya tano iliyokuwa nayo mwaka 2025, Kushuka huko kunahusishwa na mwenendo wao katika CAF Champions League, ambapo walimaliza mkiani mwa kundi D na kushindwa kusonga mbele kwa kutoka hatua ya makundi ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa misimu kadhaa mfululizo walioshiriki mashindano hayo.
Wakati Simba ikiporomoka, wapinzani wao wa jadi Yanga Afrika wamepanda wakifikia nafasi ya 12 wakiwa na alama 35, hali inayoashiria ushindani mkali wa klabu za Tanzania katika ramani ya soka la Afrika.
Kwa upande mwingine, Azam FC imepiga hatua na kufika nafasi ya 38 sambamba na Singida Black Stars, kufuatia mwenendo mzuri waliouonyesha katika mashindano ya CAF Confederation Cup kwa kucheza hatua ya makundi kwa mara Yao ya kwanza.
Kwa ujumla, hali hii inaonyesha kuwa licha ya changamoto, klabu za Tanzania zinaendelea kupambana kujenga ushindani katika michuano ya kimataifa, huku zikihitaji kuongeza ubora na uthabiti ili kurejea kwenye nafasi za juu barani Afrika.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment