SIMBA CHALII SHAURI LA DAMARO

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Simba SC imeshindwabkufua dafu baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutupilia mbali shauri lao dhidi ya uhalali wa mchezaji Mohamed Damaro Camara.

Simba waliwasilisha malalamiko wakidai kuwa usajili wa Camara haukuwa halali, wakieleza kuwa Yanga Africans walikiuka kanuni kwa kuwa na wachezaji 13 wa kigeni badala ya 12 wanaoruhusiwa kisheria.

Hata hivyo, Kamati hiyo imebaini kuwa hakuna ukiukwaji wa kanuni zilizowasilishwa na Simba, ikisisitiza kuwa usajili wa Camara ulikuwa halali kwa mujibu wa taratibu za ligi na kanuni za FIFA.

Kwa mujibu wa uamuzi huo, Simba sasa wana nafasi ya kukata rufaa kama hawajaridhika, hatua ambayo inaweza kupeleka suala hilo katika ngazi ya juu zaidi ya kisheria ndani ya mpira wa miguu.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments