Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kocha Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola, amethibitisha kuwa kiungo wake mahiri Bernardo Silva ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu wa ligi.
Guardiola amesema kuwa uamuzi wa Silva ni wa binafsi, huku akisisitiza kuwa klabu inaheshimu maamuzi ya mchezaji huyo ambaye ameitumikia timu kwa mafanikio makubwa kwa kipindi chote alichokuepo klabuni hapo.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno amekuwa mhimili muhimu wa kikosi cha City, akichangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya kutwaa mataji mbalimbali ya Ligi Kuu ya England pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kuondoka kwake kunatarajiwa kuacha pengo katika safu ya kiungo ya timu hiyo, jambo linaloweza kuathiri mfumo na ubunifu wa kikosi hicho kinachotegemea sana uwezo wake wa kuchezesha timu.
Hata hivyo, uongozi wa Manchester City unaelezwa kuanza mipango ya kusaka mbadala sahihi wa kuziba nafasi hiyo muhimu, huku mashabiki wakingojea kuona hatma ya kikosi hicho baada ya kuondoka kwa mmoja wa wachezaji wake tegemeo.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment