SERENGETI BOYS KAZINI AFCON U-17 2026

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania, maarufu kama Serengeti Boys, inatarajiwa kushiriki michuano ya AFCON U-17 Morocco 2026 itakayofanyika nchini Morocco ambapo imepangwa kundi C pamoja na timu za Mali, Angola na Mozambique.

Michuano hiyo mikubwa ya vijana barani Afrika, iliyoandaliwa na CAF, inatarajiwa kuanza rasmi Mei 13 na kumalizika Juni 2, 2026, huku ikikusanya mataifa 16 kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 .

Serengeti Boys wanaingia katika mashindano hayo wakiwa na dhamira ya kufanya vizuri na kuiwakilisha vyema Tanzania katika jukwaa hilo la kimataifa, huku wadau wa soka nchini wakisubiri kuona kiwango cha vijana hao katika ushindani wa hali ya juu.

Hakuna hofu kuhusu uwezo wa vijana watanzania kutokana na historia ya timu hiyo katika mashindano hayo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments