Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mwamuzi wa kimataifa kutoka Somalia, Omar Artan, ameteuliwa na FIFA kuwa miongoni mwa waamuzi watakaochezesha Fainali za Kombe la Dunia 2026, hatua inayothibitisha kupanda kwa kiwango chake katika uamuzi wa soka kimataifa.
Uteuzi wake unatajwa kuwa wa kihistoria, ukiakisi imani ya FIFA kwa mwamuzi huyo kutoka ukanda wa Afrika Mashariki, huku ukizingatia uzoefu na utendaji wake mzuri katika mashindano ya kimataifa.
Mbali na Artan, waamuzi wengine kutoka Afrika walioteuliwa ni:
Mustapha Ghorbal (Algeria)
Amin Mohamed (Misri)
Pierre Atcho (Gabon)
Jalal Jayed (Moroccan football referee)
Dahane Beida (Mauritania)
Tom Abongile (Afrika Kusini)
Uteuzi huu unaonesha ushindani na ubora wa waamuzi wa Afrika katika jukwaa la kimataifa, na hii inawakumbusha waamuzi kutoka kuwa makini wanapofanya maamuzi hususani kwenye michezo mikubwa na kutenda haki ili kuongeza imani kimataifa.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment