NYOTA SITA MADRID HATARINI KUUKOSA MCHEZO WA MARUDIANO DHIDI YA BAYERN

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Real Madrid inaweza kuingia kwenye pigo kuelekea mchezo wa marudiano wa UEFA Champions League hatua ya robo fainali dhidi ya Bayern Munich, baada ya wachezaji wake sita kuwa hatarini kusimamishwa kufuatia kuwa na kadi za njano.

Nyota waliopo kwenye hatari hiyo ni Kylian Mbappe, Aurelien Tchouameni, Jude Bellingham, Vinicius Junior , Alvaro Carreras pamoja na Dean Huijsen.

Wachezaji hao wote wameonyeshwa kadi za njano katika michezo iliyopita, na endapo watapata kadi nyingine katika mchezo wa Leo robo fainali ya kwanza basi , watakosa moja kwa moja mchezo wa marudiano hali inayoweza kuiathiri Real Madrid.

Kocha wa kikosi hicho anatarajiwa kusisitiza nidhamu na umakini mkubwa kwa wachezaji wake ili kuepuka adhabu hiyo muhimu, hasa ikizingatiwa uzito wa mchezo dhidi ya wapinzani wao Bayern Munich.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments