Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Beki wa kushoto wa Liverpool FC, Andy Robertson, amethibitisha kuwa ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu, akihitimisha safari ya mafanikio ya miaka tisa ndani ya Anfield.
Nyota huyo wa kimataifa wa Scotland ameacha alama kubwa ndani ya klabu hiyo, akisisitiza kuwa ataendelea kujitoa kwa nguvu zote hadi siku yake ya mwisho, licha ya uamuzi wa kuagana na timu hiyo aliyoiita kila kitu kwake.
Katika kipindi chake akiwa Liverpool tangu mwaka 2017, Robertson amefanikiwa kuisaidia timu hiyo kutwaa mataji makubwa na kuirejesha kwenye ubora wa juu barani Ulaya na England.
Mafanikio anayoyaacha Robertson Liverpool ni pamoja na:
Ubingwa wa UEFA Champions League (1)
Ubingwa wa Premier League (2)
Kombe la FA Cup (1)
Kombe la EFL Cup (2)
FIFA Club World Cup (1)
UEFA Super Cup (1)
FA Community Shield (1)
Robertson ataondoka akiwa ni mmoja wa mabeki bora waliowahi kuivaa jezi ya Liverpool, huku mchango wake wa pasi za mabao, kasi na mapambano uwanjani ukiendelea kukumbukwa na mashabiki wa klabu hiyo.
Kuondoka kwake kunaashiria mwisho wa enzi ya kizazi cha wachezaji waliolirejesha jina la Liverpool katika ramani ya soka la dunia.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment