Kutoka kileleni hadi shimoni, Leicester City yaandika historia ya maumivu

 


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Ni simulizi ya kushangaza na yenye majonzi makubwa katika soka la kisasa ambapo Klabu ya Leicester City, iliyotikisa dunia kwa kubeba taji la Premier League mwaka 2016, sasa imejikuta ikishuka hadi daraja la tatu, EFL League One mwaka 2026.

Mwaka 2016 ulikuwa wa kihistoria kwa “The Foxes” chini ya kocha Claudio Ranieri, wakiongozwa na nyota kama Jamie Vardy na Riyad Mahrez Walifanya kile kilichoonekana kama muujiza, wakitwaa ubingwa dhidi ya vigogo wa soka la England.

Baada ya mafanikio hayo, Leicester waliendelea kushiriki mashindano makubwa barani Ulaya ikiwemo UEFA Champions League, wakionesha kuwa si timu ya kubahatisha bali yenye ushindani wa hali ya juu.

Hata hivyo, miaka kumi baadaye, hali imebadilika kwa kasi ya kushangaza, Kushuka kwa kiwango cha timu, mabadiliko ya makocha, pamoja na changamoto za kiuchumi na kiutawala zimepelekea anguko hili kubwa, Hatimaye, mwaka 2026, Leicester wanajikuta wakishuka hadi daraja la tatu , hatua inayochora moja ya anguko kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa kwenye soka la kisasa.



Kutoka muujiza wa mwaka 2016 hadi simanzi ya mwaka 2026, safari ya Leicester City ni ukumbusho kwamba katika soka, mafanikio hayadumu milele leo uko kileleni, kesho unaweza kuwa chini kabisa.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments