Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kocha wa Bayern Munich Vincent Kompany ametuma ujumbe kuelekea mchezo wa marudiano nyumban dhidi ya PSG mara baada ya mchezo wa nusu fainali ya kwanza kutamatika wakipoteza 5-4 ugenini.
Kocha huyo amesisitiza umuhimu wa mashabiki kujaza uwanja wa Allianz Arena na kuipa timu nguvu ya ushindi , Kupitia mahojiano , Kompany ameweka wazi kuwa kikosi chake kiko tayari kupambana hadi mwisho.
Kompany aliwataka mashabiki wa FC Bayern Munich kuhakikisha wanakuwa katika hali bora siku ya mchezo, akisisitiza kuwa yeyote asiyejisikia vizuri abaki nyumbani na kumpa nafasi shabiki mwenye nguvu zaidi kuhudhuria, Lengo ni kuhakikisha mashabiki 75,000 wanajaza uwanja na kuigeuza Allianz Arena kuwa ngome imara kwa timu yao.
Kocha huyo aliongeza kuwa timu yake inahitaji msaada mkubwa kutoka kwa mashabiki, akisema kuwa wanapaswa “kucheza pamoja” ili kufanikisha ushindi. Alisisitiza kuwa hali ya uwanjani itakuwa ya kipekee na ya msisimko mkubwa, huku wachezaji wakiwa tayari kutoa kila walicho nacho.
Kwa kauli yenye uzito mkubwa, Kompany alisema: “Tutaacha kila kitu uwanjani, tuko tayari kufa uwanjani kama itahitajika.” Kauli hiyo inaonyesha dhamira na ari ya juu ya kikosi hicho katika kuhakikisha wanapata matokeo chanya.
Katika hitimisho lake, Kompany alitoa ujumbe wa matumaini akisema: “Bado haijaisha. Tunaamini tunawasubiri wao.” Kauli inayodhihirisha imani kubwa ya timu kuelekea pambano hilo muhimu.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment