KISA KUITAMANI MADRID ENZO AFUNGIWA MICHEZO MIWILI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

“Ningependa kuishi Madrid, ni jiji zuri sana na linanikumbusha nyumbani Buenos Aires" kauli ya Enzo Fernandez iliyoibua mjadala mkubwa na hatimaye kumuingiza kwenye adhabu ya kufungiwa michezo miwili na klabu yake ya Chelsea.

Kiungo huyo amepewa adhabu hiyo kufuatia matamshi yaliyotafsiriwa kama kuonyesha wazi kuvutiwa na Real Madrid, jambo ambalo halikupokelewa vyema na uongozi pamoja na mashabiki wa timu yake hivyo kupelekea kuadhibiwa kukosa michezo miwili dhidi ya Port Vale robo fainali FA, na dhidi ya Man city mchezo wa EPL.

Taarifa zinaeleza kuwa kauli hiyo ilitolewa katika mahojiano ya hivi karibuni na chombo kimoja cha habari ambapo nyota huyo alizungumzia uzuri wa jiji la Madrid na hata kuashiria uwezekano wa kuishi huko siku zijazo, hali iliyochukuliwa kama kuvunja misingi ya nidhamu ya ndani ya timu.

Hatua hiyo imechukuliwa kama mchezaji kuwa tayari kujiunga na klabu kufuatia tetesi za kuhusishwa kujiunga na klabu hiyo ikiwa ni miongoni mwa wachezaji wanaofuatiliwa kwa karibu kwaajili ya kuongeza nguvu.

Hatua hiyo ya kinidhamu inalenga kulinda heshima na utulivu wa kikosi, hasa katika kipindi hiki muhimu cha mashindano, huku tukio hilo likiendelea kuzua maswali juu ya mustakabali wa Enzo ndani ya klabu yake.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com




0/Post a Comment/Comments