Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Timu ya taifa ya Italia imeendelea kuporomoka kimataifa baada ya kushindwa kufuzu Kombe la Dunia kwa mara ya tatu mfululizo, kufuatia kuondolewa na Bosnia and Herzegovina katika hatua ya mchujo.
Italia, ambayo mara ya mwisho kushiriki fainali za Kombe la Dunia ilikuwa mwaka 2014, ilishindwa kutamba tena licha ya kuwa na kikosi chenye wachezaji wa kiwango cha juu wanaocheza katika ligi kubwa barani Ulaya.
Katika mchezo huo muhimu, Italia ilijikuta ikitolewa kwa mikwaju ya penalti 4-1 baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika za kawaida, huku Bosnia and Herzegovina wakionyesha uimara mkubwa na kuibuka na ushindi uliowapeleka kombe la Dunia.
Matokeo hayo yanaifanya Italia kuendeleza rekodi mbaya ya kukosa fainali za Kombe la Dunia tangu mwaka 2018, 2022 hadi sasa 2026, jambo linaloibua maswali mengi kuhusu mwelekeo wa soka la taifa hilo lenye historia kubwa duniani.
Pamoja na uwekezaji mkubwa na uwepo wa vipaji lukuki, kushindwa huku kunaweka wazi kuwa Italia inahitaji mabadiliko makubwa ili kurejesha makali yake na heshima yake katika soka la kimataifa.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment