Enzo Fernandez arejea kikosini baada ya kuomba radhi

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kiungo wa Enzo Fernandez anatarajiwa kurejea katika kikosi cha Chelsea FC ndani ya wiki hii, kufuatia hatua yake ya kuomba radhi kwa benchi la ufundi pamoja na wachezaji wenzake.

Taarifa hiyo imekuja baada ya mazungumzo ya ndani yaliyohusisha uongozi wa timu, huku kocha Liam Rosenior akieleza kuwa kiungo huyo tayari amekamilisha mchakato wa kusuluhisha tofauti zilizokuwepo.

“Enzo amezungumza nami, kundi la viongozi na wachezaji wote, na sasa tunatazamia kumkaribisha tena,” alisema Rosenior, akisisitiza kuwa mchezaji huyo alionesha nia ya dhati ya kurekebisha hali.

Kocha huyo aliongeza kuwa Fernandez mwenyewe aliomba kukutana na viongozi wa timu pamoja na wachezaji ili kuweka mambo sawa, jambo lililosaidia kufungua ukurasa mpya ndani ya klabu hiyo ya London.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments