EKITIKE KULIKOSA KOMBE LA DUNIA ATAKUWA NJE HADI JANUARY 2027

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Ufaransa, Hugo Ekitike, anatarajiwa kukosa michuano ya Kombe la Dunia kufuatia kupata jeraha kubwa la mshipa mkubwa uliopo nyuma ya kifundo Cha mguu katika mchezo wa robo fainali ya UEFA Champions League dhidi ya PSG, ambapo Liverpool ilipoteza kwa mabao 2-0 na kuondoshwa kwenye mashindano hayo.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka kwa madaktari wa klabu hiyo, vipimo vya kitabibu vilivyofanyika vimethibitisha kuwa nyota huyo amepata jeraha kubwa la mshipa unaounganisha mfupa wa kisigino (Achilles tendon). Jeraha hilo linatajwa kuhitaji muda mrefu wa matibabu na uangalizi, huku akitarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi tisa, hadi Januari 2027.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa jeraha hilo ni pigo kwa Liverpool, kutokana na umuhimu wa mchezaji huyo katika safu ya ushambuliaji, sambamba na kuwa hasara kwa timu ya taifa ya Ufaransa katika mashindano yajayo ya kombe la Dunia.

Hata hivyo, wachezaji wenzake, benchi la ufundi pamoja na mashabiki wameendelea kutuma jumbe za kumtia moyo, wakiamini kuwa ataweza kurejea uwanjani akiwa imara zaidi baada ya kukamilisha mchakato wa matibabu na urejeaji wa kiwango chake.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments