Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Droo ya hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la CRDB imefanyika Aprili 17, 2026 jijini Dar es Salaam.
Katika ratiba hiyo, Simba SC watakutana na TRA United katika dimba la Meja Jenerali Isamuhyo, huku mabingwa watetezi Young Africans SC wakipewa kibarua kizito dhidi ya JKT Tanzania.
Michezo mingine itashuhudia Azam FC wakisafiri hadi Kigoma kuvaana na Mashujaa FC kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, wakati Coastal Union wakialikwa na Singida Black Stars katika dimba la Mkwakwani, Tanga.
Kwa mujibu wa upangaji huo, washindi wa mechi kati ya Simba SC na TRA United watakutana na mshindi wa Coastal Union dhidi ya Singida Black Stars katika hatua ya nusu fainali. Upande mwingine, mshindi wa Azam FC na Mashujaa FC atamenyana na atakayevuka kati ya JKT Tanzania na Young Africans SC.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment