Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Timu ya taifa ya DR Congo imefanikiwa kufuzu kushiriki FIFA World Cup 2026, baada ya kuwanyuka Jamaica 1-0 kwenye mchezo ulipigwa nchini Mexico kwa bao la la dk 100' lililowekwa kimiani na Alex Tuanzebe.
Imechukuwa zaidi ya miaka 52 kwa Congo kurejea tena katika mashindano hayo ambapo mara ya mwisho kushiriki ilikuwa ni mwaka 1974, sasa Afrika inafikiasha Jumla ya timu 10 , zitakazo shiriki kombe la Dunia mwaka huu, ambalo litapigwa kwa ushirikiano wa nchi tatu Marekani, Canada na Mexico.
Katika hatua ya upangaji wa makundi, DR Congo imedondokea Kundi K pamoja na timu za Portugal , Uzbekistan na Colombia.
DR Congo wameingia kwenye hatua nyingine muhimu yakwenda kuandika historia mpya licha ya kupangwa kundi lenye vigogo lakini haimaanishi hawawezi kuwafunga, jitihada na mbinu za mwalimu zitawafanya kuonyesha mshangao katika mashindano hayo.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment