Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Timu ya mpira wa kikapu ya Dar City imeandika historia mpya baada ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Basketball Africa League 2026 kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake, ikiwa ni mafanikio makubwa kwa mchezo wa kikapu nchini Tanzania.
Licha ya kupoteza mchezo wao wa mwisho kwa alama dhidi ya Tigers, Dar City walifanikiwa kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa kundi, matokeo yaliyowatosha kusonga mbele kwa faida ya head-to-head dhidi ya Nairobi City Thunder.
Safari ya Dar City imekuwa ya kuvutia huku wakionyesha ushindani mkubwa dhidi ya timu zenye uzoefu mkubwa barani Afrika, jambo linaloashiria ukuaji wa kiwango cha kikapu Tanzania na kuipa heshima kimataifa.
Hatua ya robo fainali inatarajiwa kufanyika jijini Kigali kuanzia Mei 22 hadi Mei 31, 2026, ambapo Dar City watapata nafasi nyingine ya kuendelea kuweka historia na kuiwakilisha Tanzania katika jukwaa la kimataifa.
Mashabiki wa kikapu nchini sasa wana kila sababu ya kujivunia mafanikio haya, huku macho yakielekezwa Kigali kuona kama Dar City wataendelea kung’ara na kufika hatua za juu zaidi za mashindano hayo makubwa barani Afrika.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com m


Post a Comment