Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Chelsea imeamua kumtimua kocha mkuu Liam Rosenior baada ya kuiongoza timu hiyo kwenye mwendo mbaya wa michezo mitano mfululizo ya Ligi Kuu England bila ushindi, huku ikipoteza yote na kushindwa kufunga bao hata moja.
Mfululizo huo mbaya umejumuisha vipigo dhidi ya Newcastle, Everton, Manchester City, Manchester United na mchezo wa mwisho dhidi ya Brighton, hali iliyozua presha kubwa kutoka kwa mashabiki na uongozi wa klabu.
Baada ya matokeo hayo mabaya, taarifa zimeeleza kuwa kocha wa timu ya vijana chini ya miaka 21, Calum McFarlane, amekabidhiwa jukumu la kuinoa timu hiyo kama kocha wa muda hadi mwisho wa msimu.
McFarlane si mgeni katika nafasi hiyo, kwani aliwahi kuiongoza Chelsea kwa muda mfupi mapema mwaka huu baada ya kuondoka kwa Enzo Maresca, kabla ya Rosenior kuteuliwa rasmi. Sasa amepewa tena jukumu la kuokoa msimu wa The Blues huku klabu hiyo ikianza mchakato wa kutafuta kocha mpya wa kudumu kwa msimu wa 2026/27.
Mashabiki wengi wa Chelsea wameonyesha kutoridhishwa na kiwango cha timu, hasa kutokana na ukame wa mabao na kuporomoka kwa nafasi kwenye msimamo wa ligi, jambo lililopelekea uongozi kuchukua uamuzi huo mgumu.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment