BRUNO AKARIBIA KUVUNJA HISTORIA PASI ZA MAGOLI EPL

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kiungo mshambuliaji wa Manchester United, Bruno Fernandes, ameendelea kung’ara katika Premier League baada ya kufikisha jumla ya pasi za mabao (assist) 19 ndani ya msimu wa 2025/26.

Fernandes alifikia mafanikio hayo kufuatia kutoa assist katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Brentford ambapo mchango wake uliendelea kuwa chachu ya mafanikio kwa United msimu huu.

Kwa sasa, nyota huyo wa Ureno yupo nyuma kwa assist moja tu kufikia rekodi ya muda wote ya msimu mmoja inayoshikiliwa na Thierry Henry na Kevin De Bruyne, waliowahi kufikisha assist 20 kila mmoja ,akiwa na michezo minne iliyosalia, Fernandes ana nafasi kubwa ya kuandika historia mpya.

Iwapo atafikisha assist 20, atalingana na mastaa hao wawili, lakini akifanikiwa kufikisha assist 21, ataweka rekodi mpya ya kipekee katika historia ya Premier League na endapo hataongeza idadi hiyo, atasalia katika nafasi ya tatu ya wachezaji waliotoa assist nyingi zaidi kwa msimu mmoja.

Kwa kasi yake ya sasa, macho ya mashabiki na wadau wa soka duniani yataendelea kumtazama Fernandes kuona kama ataandika historia mpya au ataishia kuwa miongoni mwa wabunifu bora kuwahi kushuhudiwa katika ligi hiyo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments