BILIONI 400 KUIMARISHA SEKTA YA SANAA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Naibu Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma, amesema Serikali imepanga kutekeleza mradi wa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa Arena pamoja na studio za kisasa za filamu nchini, hatua inayolenga kukuza na kuimarisha sekta ya sanaa.

Akizungumza Bungeni jijini Dodoma, Mwinjuma alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Makete, Festo Sanga, aliyekuwa akitaka kujua maendeleo ya mradi huo wa Arena.

Katika ufafanuzi wake, Mwinjuma alisema kuwa Serikali tayari imeweka takribani shilingi bilioni 400 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa. Alibainisha kuwa fedha hizo ni mkopo wenye masharti nafuu uliotolewa na Benki ya Exim ya Korea.

Aidha, alisisitiza kuwa maandalizi ya awali yamekamilika kwa kiasi kikubwa, na kwamba ujenzi wa miundombinu hiyo muhimu unatarajiwa kuanza hivi karibuni ili kufanikisha azma ya kuinua tasnia ya sanaa nchini.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments