Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Bayern Munich imeonyesha ubabe wake katika soka la Ujerumani baada ya kutwaa ubingwa wa Bundesliga kwa mara ya 34, ikiwa bado na michezo minne mkononi.
Bayern wanatwaa taji hilo mapema kufuatia ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya VfB Stuttgart, matokeo yaliyowafikisha alama 79 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote iliyosalia katika mbio za ubingwa msimu huu.
Katika msimamo wa ligi, Borussia Dortmund wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na alama 64 baada ya michezo 30, kwa alama hizo hawawezi kufikia alama za Bayern Hata wakishinda michezo yao yote iliyobaki kwani watafikisha alama 76 pekee idadi ambayo bado iko nyuma ya Bayern.
Ushindi huu unaendelea kudhihirisha uimara wa Bayern Munich, klabu ambayo imekuwa nguzo kuu ya mafanikio katika Bundesliga kwa miaka mingi. Kutwaa ubingwa huku wakiwa bado na michezo minne mkononi ni ishara tosha ya ubora wao na pengo kubwa waliloweka dhidi ya wapinzani wao.
Kwa mara nyingine tena, Bayern Munich wameandika historia mpya na kuendelea kuthibitisha hadhi yao kama watawala wa soka la Ujerumani na hawaja chukua kwa bahati mbaya bali ni uwezo wao ambapo hata kwenye mashindano ya Ulaya UCL wapo hatua ya nusu fainali , hivyo huenda ukawa ni msimu wa mafanikio zaidi ikiwa watachukuwa na UCL.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment