BAYERN KUMREJESHA JACKON THE BLUES

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mshambuliaji wa Chelsea Nicolas Jackson anatarajiwa kurejea katika kikosi hicho ifikapo mwezi Juni baada ya kumaliza mkopo wake ndani ya Bayern Munich, hiyo imekuja baada ya Bayern kusitisha mpango wa kutumia kipengele cha kumnunua kilichokadiriwa kufikia euro milioni 65.

Awali, kulikuwa na matarajio makubwa ya nyota huyo kuhamia Allianz Arena, lakini mambo yalibadilika ghafla baada ya uongozi wa Bayern kuamua kujiondoa kwenye dili hilo uamuzi huo ulithibitishwa na mkurugenzi wa klabu hiyo, Max Eberl, alipokuwa akizungumza na kituo cha ZDF, akieleza kuwa klabu hiyo imepiga hesabu upya kuhusu mwelekeo wa usajili wao.

Kutokana na mabadiliko hayo, sasa upepo umegeuka kuelekea Stamford Bridge, ambapo Chelsea pamoja na wawakilishi wa Jackson wanatarajiwa kukaa mezani kujadili mustakabali wake.

Hata hivyo, pamoja na kurejea kwake, bado kuna uwezekano wa mazungumzo mapya ya uhamisho kufunguliwa, hasa kama ataonyesha kiwango bora katika kipindi kilichosalia cha msimu.

Kwa mtazamo wa ushindani, hatua hii inaweza kuwa na athari kubwa kwa safu ya ushambuliaji ya Chelsea, huku mashabiki wakisubiri kuona kama Jackson atarejea akiwa na makali.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments