AZAM WATANGAZA VIINGILIO , SIMBA WAPINGA WADAI NI GHALI

 


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Azam FC imetangaza viingilio kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya Simba SC utakaopigwa Aprili 5, 2026 katika dimba la Azam Complex, huku bei hizo zikizua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wa soka nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Aprili 4, 2026, kiingilio cha chini (mzunguko) kimetangazwa kuwa Shilingi 15,000, huku VIP B ikiwa 25,000 na 30,000 kwa VIP A. Hatua hiyo imeibua hisia tofauti hasa kutokana na gharama za usafiri kwa mashabiki wanaotarajiwa kusafiri hadi uwanjani ukijumlisha na gharama za tiketi inakuwa gharama kubwa.

Upande wa Simba SC kupitia Meneja wa Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally, umepinga vikali viingilio hivyo ukidai ni mpango wa kuwanyima mashabiki wao fursa ya kushuhudia mchezo huo muhimu.

Ahmed Ally amesema licha ya Azam kuwa wenyeji wa mchezo huo, lakini kiwango cha chini cha kiingilio cha Shilingi 15,000 hakijawahi kuwekwa katika michezo ya aina hiyo, akisisitiza kuwa hatua hiyo inaweza kuathiri mahudhurio ya mashabiki uwanjani.

Mara nyingi Viingilio vya mzunguko huwa 5000 kiingilio ambacho huchukuliwa kama rafiki kwa mashabiki Wengi hapa nchini.

Mjadala kuhusu viingilio hivyo unaendelea kushika kasi huku wadau wa soka wakisubiri kuona kama malaka za usimamizi wa ligi zitakuja na tamko au kutakuwa na mabadiliko au msimamo utaendelea kuwa ule ule kuelekea mchezo huo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com


0/Post a Comment/Comments