ARSENAL YAONDOSHWA FA CUP, NDOTO YA TREBLE YAZIMIKA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Ndoto ya mafanikio makubwa ndani ya msimu mmoja kwa Arsenal imeendelea kugonga mwamba baada ya kuondoshwa katika hatua ya robo fainali ya FA Cup kufuatia kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Southampton.

Matokeo hayo yanamaanisha kuwa Arsenal wamepoteza mashindano ya pili mfululizo ndani ya kipindi kifupi, baada ya siku chache zilizopita kukubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Manchester City katika Fainali ya Carabao Cup.

Kuporomoka huko kumefuta rasmi ndoto ya kutwaa mataji matatu (treble) msimu huu, jambo ambalo lilionekana linawezekana kutokana na mwanzo wao mzuri katika mashindano waliyokuwa wakishiriki.

Kwa sasa, matumaini ya Arsenal yamebaki kwenye mashindano mawili makubwa pekee ambayo ni English Premier League pamoja na UEFA Champions League, ambapo wanahitaji kurejea kwenye kiwango chao bora ili kuokoa msimu wao ambapo asilimia kubwa ipo kwenye kutwaa EPL na kuhusu UEFA inategemea upambanaji wao na mbinu za mwalimu dhidi ya wapinzani wake.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments