Arsenal yageuzwa juu chini, City yaukaribia ubingwa

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Arsenal imejikuta ikiingia kwenye wakati mgumu katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Manchester City katika mchezo mkali uliopigwa dimba la Etihad leo, Aprili 19, 2026.

Mchezo huo uliokuwa na uzito mkubwa katika kuamua hatima ya ubingwa, uliwakutanisha vinara hao wawili katika mbio za ubingwa huku Arsenal wakiwa juu ya msimamo kwa tofauti ya alama tatu baada ya kichapo hicho.

Kwa matokeo hayo, Manchester City sasa ipo kwenye nafasi nzuri ya kupanda kileleni endapo itaibuka na ushindi katika mchezo wake wa Jumatano dhidi ya Burnley, ambapo kama watashinda wataongoza kwa faida ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Mbio za ubingwa sasa zimeingia katika hatua ya mwisho yenye presha kubwa, huku Arsenal wakibakiwa na michezo mitano dhidi ya Newcastle United, Fulham, West Ham United, Burnley na Crystal Palace.

Kwa upande wa Manchester City, wao watashuka dimbani katika michezo sita iliyosalia wakikabiliana na Burnley, Everton, Brentford, AFC Bournemouth, Crystal Palace na Aston Villa.

Ikiwa timu zote mbili zitafanikiwa kushinda michezo yao yote iliyosalia, ubingwa wa msimu huu utaamuliwa kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa hali inayoongeza presha na ushindani mkali zaidi katika hatua za mwisho za ligi.

Kwa sasa, kila kosa linaweza kuwa la mwisho, na mashabiki wa soka duniani wanashuhudia moja ya mbio za ubingwa zenye mvuto mkubwa kuwahi kutokea.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments