Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Arsenal imeandika historia baada ya kuihakikishia Premier League nafasi ya ziada katika UEFA Champions League, hatua inayomaanisha kuwa timu tano bora zitashiriki michuano hiyo msimu wa 2026/2027.
Mafanikio hayo yamechangiwa na matokeo mazuri ya Arsenal katika mashindano ya Ulaya ikichagizwa na ushindi wa 1-0 walioupata ugenini dhidi ya Sporting CP kwenye robo fainali ya kwanza Uefa, na kufanya ligi ya England kukusanya alama za kutosha kwenye viwango vya UEFA na hivyo kupata nafasi ya juu barani humo.
Kwa mujibu wa utaratibu wa UEFA, ligi mbili zitakazoongoza kwa alama hizo hupata nafasi ya ziada ya kuiwakilisha Ulaya kwenye Champions League, ambapo sasa Premier League imefanikiwa kupata nafasi hiyo adhimu.
Hatua hiyo inaongeza ushindani mkubwa katika msimamo wa ligi, huku timu zitakazomaliza nafasi tano za juu zikipata tiketi ya moja kwa moja kushiriki michuano hiyo mikubwa zaidi ya vilabu barani Ulaya.
Kwa sasa, mbio za kuwania nafasi hizo zinaendelea kupamba moto zikihusisha vilabu vikubwa kama Manchester City, Manchester United, Liverpool , Aston Villa na Chelsea.
0767815473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment