YANGA SARE YA TATU MFULULIZO , MASHABIKI WALIA NA UMALIZIAJI NAFASI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Young Africans imeendelea kupunguza kasi katika mbio za ubingwa baada ya kudondosha alama sita muhimu kufuatia sare tatu mfululizo katika michezo ya hivi karibuni ya NBC Premier League.

Yanga ilianza kwa kutoka sare tasa ya 0-0 dhidi ya Azam fc kabla ya kurudia matokeo hayo dhidi ya TRA, na Katika mchezo wa leo, mabingwa hao walishindwa tena kupata ushindi baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar wakatamiwa kutokea turiani Morogoro.

Matokeo hayo yamezua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki, wengi wakieleza kutoridhishwa na kiwango cha timu hiyo, hususan katika safu ya ushambuliaji, Licha ya benchi la ufundi linaloongozwa na Pedro Goncalves kueleza kuwa majeraha ya wachezaji yameathiri kikosi, mashabiki wanaamini tatizo kubwa ni kukosa umakini wanapopata nafasi za kufunga.

Katika mchezo wa leo, wachezaji kama Pacome Zouzoua pamoja na Mwanengo walipata nafasi za wazi katika dakika za jioni ambazo zingeweza kuipa timu ushindi, lakini walishindwa kuzitumia ipasavyo.

Aidha, taarifa ya kitabibu kutoka klabuni hapo iluthibitisha kuwa wachezaji kadhaa muhimu wapo nje kutokana na majeraha, hali inayozidi kuongeza presha katika kikosi hicho.

 Miongoni mwao ni Ibrahim Abdullah Bacca, Laurindo Dilson Depu, Chadrack Boka na Edmund John ambao wote wanatarajiwa kuukosa uwanja kwa takriban wiki mbili, wengine wakiwa ni Clement Mzize na Dickson Job.

Kutokana na mwenendo huo, presha inaendelea kuongezeka ndani ya klabu hiyo huku mashabiki wakitaka maboresho ya haraka ili kurejesha matumaini ya kutetea ubingwa wao msimu huu.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments