YAFAHAMU MASHINDANO YA FIFA SERIES

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mashindano ya kimataifa ya FIFA Series yameanza kushika kasi duniani tangu yalipozinduliwa rasmi na Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, mnamo mwaka 2024, yakilenga kuongeza ushindani na fursa kwa mataifa mbalimbali kujipima uwezo.

Kupitia mashindano hayo, timu kutoka mabara tofauti hukutana katika vituo maalum na kucheza michezo ya kirafiki yenye ushindani mkubwa, hatua inayolenga kuzisaidia hasa nchi zinazoendelea kisoka ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikikosa michezo yenye ushindani wa uhakika.

Kwa mujibu wa FIFA, mpango huo unakusudia kupunguza pengo la viwango kati ya mataifa makubwa na madogo, huku ukitoa nafasi kwa wachezaji kupata uzoefu wa kimataifa na makocha kupima vikosi vyao katika mazingira tofauti ya ushindani na kubadilishana utamaduni baina ya taifa na taifa.

Mbali na hilo, mashindano hayo yanatarajiwa kuwa sehemu ya kalenda ya kudumu ya soka la kimataifa, yakifanyika kila mwaka unaogawika kwa mbili ( Even number) jambo litakalosaidia kuongeza mwendelezo wa michezo ya kirafiki yenye tija na kuvutia mashabiki wengi zaidi duniani.

0767915474,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments