UTATA WA BAO LA SIMBA WAZUA MASWALI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kauli ya bao halali halafu kukataliwa iliyotolewa katika taarifa ya Bodi ya Ligi imezua maswali mengi kwa wadau wa soka.

Kupitia Afisa Habari wake Karim Boimanda, Bodi ya Ligi ilieleza kuwa mwamuzi alikataa bao halali la Simba katika mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga uliochezwa wikiendi iliyopita visiwani Zanzibar.

Hata hivyo kauli hiyo imeibua mjadala, huku wengi wakihoji kuwa kwa mujibu wa sheria za soka, mwenye mamlaka ya kuamua kama goli ni halali au si halali ni mwamuzi wa mchezo, na si Bodi ya Ligi.

Kutokana na hilo, wadau wasoka nchini wamewashauri bodi ya ligi kuwa makini wakati wanatoa taarifa zao ikiwa ni kuzingatia kanuni ili kuepusha mijadala na sintofahamu kwa upande fulani.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments