Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa maandalizi ya FIFA World Cup 2026 yanaendelea vizuri huku akiahidi kuwa mashindano hayo yatakuwa miongoni mwa matukio makubwa na salama zaidi katika historia ya michezo nchini Marekani.
Trump amesema michuano hiyo, itakayoandaliwa kwa ushirikiano kati ya United States, Canada na Mexico, imepewa kipaumbele kikubwa na serikali yake ili kuhakikisha inakuwa na mafanikio makubwa na usalama wa kutosha kwa mashabiki na timu zitakazoshiriki.
Akizungumzia maandalizi hayo, Trump alieleza kuwa tayari kikosi maalum kimeanzishwa katika Ikulu ya Marekani kwa ajili ya kuratibu juhudi zote za maandalizi ya mashindano hayo.
Kikosi hicho kinatarajiwa kushirikiana na wizara na taasisi mbalimbali za serikali kuhakikisha maandalizi yanafanyika kwa ufanisi, huku usalama na utaratibu wa mashindano ukipewa kipaumbele kikubwa.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment