TIMU ZA EPL HATARINI KUTUPWA NJE UCL

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Ligi Kuu ya England imeingiza jumla ya timu sita katika hatua ya 16 Bora ya UEFA Champions League, lakini baada ya michezo ya mkondo wa kwanza timu nne zinaonekana kuwa kwenye hatari kubwa ya kuondolewa katika mashindano hayo.

Hatari hiyo imezikumba timu za Chelsea baada ya kupokea kipigo cha mabao 5-2 kutoka kwa PSG, huku Manchester City nao wakipoteza kwa mabao 3-0 dhidi ya Real Madrid.

Wakati huo huo Tottenham Hotspur walipata kipigo Cha mabao 5-2 kutoka kwa Atletico Madrid, huku Newcastle United wakilazimishwa sare ya 1-1 nyumbani dhidi ya FC Barcelona matokeo yanayowapa nafasi ndogo ya kusonga mbele.

Kwa upande wa timu zilizoonesha matumaini ya kufuzu kutoka England ni Arsenal ambao walipata sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Bayer Leverkusen, hivyo wana nafasi nzuri ya kumaliza kazi nyumbani, Hata hivyo kwa Liverpool nafasi yao inaonekana kuwa ya asilimia 50 kwa 50 baada ya kupoteza kwa 1-0 dhidi ya Galatasaray.

Kwa upande mwingine baadhi ya timu zimeonekana tayari kuweka mguu mmoja katika hatua ya robo fainali baada ya ushindi mkubwa katika michezo ya kwanza.

Timu hizo ni Paris Saint-Germain, Bayern Munich, Bodø/Glimt, Atlético Madrid pamoja na Real Madrid.

Michezo ya marudiano ya hatua ya 16 Bora ya UEFA Champions League inatarajiwa kupigwa Machi 17 na 18, 2026, ambapo ndipo itakapofahamika ni timu zipi zitafuzu rasmi kwenda hatua ya robo fainali.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments