Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Chelsea imepigwa marufuku ya miezi tisa kusajili wachezaji wa timu za vijana walio chini ya miaka 18 kutoka klabu za English Premier League na English Football League, pamoja na kutozwa faini ya pauni milioni 10.75.
Adhabu hiyo inatokana na ukiukaji wa sheria za kifedha uliotokea wakati wa umiliki wa Roman Abramovich kati ya mwaka 2011 hadi 2018, ikihusisha malipo ya siri ambayo hayakuripotiwa kwa mamlaka husika.
Hata hivyo, marufuku ya mwaka mmoja ya kusajili wachezaji wa kikosi cha kwanza imewekwa kama kifungo cha kusimamiwa, ikimaanisha klabu hiyo itaendelea kufanya usajili isipokiuka tena sheria hizo ndani ya kipindi hicho.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment