Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports
Mabadiliko ya sheria yanatarajiwa kuanza kutumika katika mashindano ya Kombe la Dunia, yakilenga kuongeza kasi ya mchezo na kupunguza upotevu wa muda uwanjani.
Moja ya maboresho hayo ni matumizi ya VAR, kupitiwa upya kwa kadi ya njano ya pili au kadi nyekundu endapo kutabainika kuwa kulikuwa na kosa, Hatua hiyo inalenga kuongeza usahihi wa maamuzi ya waamuzi.
Aidha, mchezaji anaye fanyiwa mabadiliko atalazimika kutoka uwanjani ndani ya sekunde 10. Iwapo atachelewa zaidi ya muda huo, mchezaji anayeingia atalazimika kusubiri mchezo uendelee mpaka mpira utakapo toka uwanjani ndio ataruhusiwa kuingia uwanjani.
Katika kupunguza mbinu za kuchelewesha muda, mchezaji atakayehitaji matibabu uwanjani atalazimika kutoka nje kwa dakika moja kabla ya kurejea kucheza.
Vilevile, waamuzi watakuwa na mamlaka ya kuhesabu sekunde tano pale watakapoona muda unapotezwa kwenye mipira ya kurushwa (throw-in) na mipira ya (goal kick), Endapo mpira hautaanzishwa ndani ya muda huo umiliki utahamishiwa kwa timu pinzani.
Marekebisho hayo yanatarajiwa kuongeza ushindani na kufanya mchezo kuwa wa kasi zaidi katika mashindano yajayo ya Kombe la Dunia hii ni kuhakikisha angalau mpira unachezwa kwa dakika zote 90.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment