Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mvutano baina ya timu ya taifa ya Senegal na shirikisho la soka barani Africa umeendeelea kuchukua Sura mpya mara baada ya timu hiyo kuendelea kukaidi wazi amri ya shirikisho mara baada ya kuendelea na sherehe za ubingwa kabla ya mchezo wao ambao waliibuka na ushindi 2-0 dhidi ya Peru kwenye uwanja wa stade de France.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Senegal walipuuzia agizo hilo na kuendelea kushikilia msimamo wao, hatua iliyozua mjadala mkubwa miongoni mwa wadau wa soka barani Afrikana Duniani kwa ujumla. Tukio hilo limeibua sintofahamu kuhusu uhalali wa maamuzi ya CAF pamoja na hatua zinazoweza kuchukuliwa dhidi ya timu hiyo.
Katika hali iliyoonekana kuongeza moto wa mjadala, Senegal waliendelea na sherehe zao katika Uwanja huo mbele ya mashabiki wao , ambapo walionyesha hadharani kombe la AFCON 2025 huku wakivaa jezi zenye nyota mbili kuashiria ubingwa wao.
Hatua hiyo imechukuliwa kama ujumbe mzito wa kutotambua uamuzi wa CAF, na sasa macho ya wengi yanaelekezwa kwa mamlaka hiyo kuona hatua itakayochukuliwa dhidi ya Senegal, huku sakata hilo likitarajiwa kuendelea kutikisa soka la Afrika kwa siku zijazo huku maamuzi ya rufaa yakisubiriwa.
0767815473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment