RONALDO JR ATUA MADRID

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

 Cristiano Ronaldo Jr, mtoto wa nyota wa zamani wa Manchester United, Juventus na Real Madrid, Cristiano Ronaldo, amefanya mafunzo ya kwanza na academy ya Real Madrid La Fabrica wiki hii, akionesha nia ya kujiunga rasmi na klabu hiyo katika siku za usoni.

Ingawa kwa sasa Cristiano Jr yupo chini ya mkataba na Al-Nasry, uwepo wake Madrid unathibitisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Ronaldo na klabu ya Hispania, Kwa mujibu wa taarifa za klabu, Christiano Jr amezingatiwa kama mchezaji mwenye kipaji cha kipekee, na anaangaliwa kwa makini kwa ajili ya siku za usoni klabuni hapo.

Cristiano Jr tayari ni sehemu ya kikosi cha taifa cha U17 cha Ureno, sambamba na kuendelea na mafunzo yake katika acafemy ya Al-Nasry, ambapo amekuwa akijengeka kiufundi , Watendaji wa Real Madrid wamesema kwamba uwepo wake La Fabrica ni hatua muhimu katika kumtengenezea njia ya kuungana na vijana wa klabu hiyo katika miaka ijayo.

Hii inakuja wakati familia ya Ronaldo inahifadhi uhusiano wa karibu na Madrid, ikionyesha matumaini ya kuendeleza urithi wa familia katika klabu hiyo, huku Christiano Jr akijipanga kuonyesha kipaji alicho nacho ili awe mchezaji wa kufuatiliwa sana katika soka la vijana duniani.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments