RONALDO HAKUKIMBIA SAUDI, AENDELEA NA MAZOEZI AL NASSR

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Nyota wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo, hajaondoka Saudi Arabia kurejea Madrid kama ilivyodaiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Ripoti zilizosambaa zilidai kuwa mshambuliaji huyo aliondoka haraka na familia yake kufuatia shambulio la bomu mjini Riyadh, Hata hivyo, taarifa za kuaminika zinaeleza kuwa Ronaldo bado yupo nchini humo akiendelea na majukumu yake ndani ya Al Nassr FC.

Kwa mujibu wa taarifa za kimataifa, tetesi zilichochewa baada ya ndege yake binafsi kuonekana ikielekea Madrid kufuatia tukio la shambulio la bomu mjini Riyadh, lakini ilithibitishwa kuwa nyota huyo hakuwa ndani ya ndege hiyo.

Badala yake, Ronaldo alionekana akiendelea na mazoezi ya timu huku pia akiwa chini ya uangalizi wa kitabibu kufuatia maumivu aliyoyapata katika mchezo uliopita , hali iliyomfanya atolewe nje wakati wa mechezo.

Hivyo, taarifa za kudai kuwa nahodha huyo alikimbia Saudi Arabia kutokana na mashambulizi zimeelezwa kuwa ni za upotoshaji, wakati klabu yake ikiendelea kufuatilia hali yake ya kiafya kabla ya kurejea uwanjani.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments