RODRI AJINASIBU ANAWEZA KUKIPIGA REAL MADRID LICHA YA KUWAHI KUITUMIKIA ATLETICO

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

KIUNGO wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Manchester City Rodri, ameibua mjadala mkubwa katika ulimwengu wa soka baada ya kuweka wazi kuwa bado anaweza kujiunga na Real Madrid licha ya historia yake ya kuitumikia Atletico Madrid.

Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja Cha habari, Rodri alisema wazi kuwa kuchezea Atlitico hakumfungii milango ya kwenda kwa wapinzani wao wa jadi, akisisitiza kuwa soka la kisasa linatoa nafasi kwa wachezaji kufanya maamuzi makubwa kulingana na mazingira na fursa.

Rodri aliendelea kuisifia Real Madrid kwa mafanikio yake ya muda mrefu, hususan katika michuano ya UEFA Champions League, akieleza kuwa ubora wa timu hiyo haupimwi kwa matokeo ya mchezo mmoja.

Aidha, alizungumzia mazingira ya uwanja wa Santiago Bernabeu akisema ni moja ya viwanja vinavyotia hofu kwa wapinzani kutokana na presha kubwa ya mashabiki wake.

Kauli hiyo imezua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki na wachambuzi wa soka, huku wengi wakiamini kuwa huenda ikawa ishara ya uwezekano wa Rodri kujiunga na Real Madrid siku zijazo huku akiwa na mkataba na City mpaka Juni ,2026.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments