Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Tottenham Hotspur imemsaini Kocha mpya raia wa Italia Roberto De Zerbi ambaye atakinoa kikosi hicho kwa mkataba wa miaka mitano akichukuwa nafasi ya Igor Tudor aliefutwa kazi kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo.
Mkataba huo unaonesha dhamira yake ya kubaki kwa muda mrefu klabuni hapo, taarifa hiyo imekuja sambamba na uthibitisho kuwa mkataba huo hauna kipengele cha kumruhusu kuondoka endapo timu itashuka daraja, ishara ya imani yake kwa mustakabali wa klabu hiyo.
De Zerbi ameielezea Tottenham kama moja ya vilabu vikubwa na vyenye heshima duniani, akisisitiza kuvutiwa kwake na historia na hadhi ya timu hiyo, amebainisha kuwa mazungumzo yake na viongozi wa klabu yalionesha wazi mipango ya kujenga kikosi imara kitakachoweza kufikia mafanikio makubwa siku za usoni.
Kocha huyo pia ameweka wazi kuwa anataka kuijenga timu itakayocheza soka la kuvutia na lenye msisimko kwa mashabiki, akiamini mtindo huo ndio utakaorejesha ushindani wa juu ndani ya klabu , ameongeza kuwa uamuzi wake wa kusaini mkataba wa muda mrefu umetokana na imani yake katika dira na malengo ya klabu.
Kwa upande wa malengo ya muda mfupi, De Zerbi ameweka wazi kuwa kipaumbele kikuu ni kupanda kwenye msimamo wa Premier League na kuhakikisha timu inafanya vizuri hadi mwisho wa msimu pia ameahidi kuwa ataweka nguvu zote katika kuhakikisha hilo linatimia.
Aidha, kocha huyo ameonyesha hamu kubwa ya kuanza kazi rasmi uwanjani kwa kushirikiana na wachezaji wake, akilenga kujenga kikosi chenye ushindani kitakachoweza kufikia malengo yaliyowekwa
076915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment