PIGO

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports ,

Klabu ya Real Madrid na timu ya Taifa ya Brazil wamepata pigo baada ya mchezaji wao Rodrygo kupata majeraha na atakuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi Saba baada ya kuumia goti katika mchezo wa ligi kuu Spain dhidi ya Getafe CF.

Rodrygo alipata jeraha hilo mapema kwenye mchezo huo na alilazimika kutolewa baada ya kucheza kwa dakika 30 pekee, jambo lililoleta taharuki kwa benchi la ufundi la Madrid pamoja na mashabiki.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu, nyota huyo wa Brazil anatarajiwa kufanyiwa matibabu na programu maalum ya uangalizi kabla ya kurejea uwanjani, huku akitarajiwa kukosa michuano mikubwa ijayo ya kombe la Dunia.

Pigo hilo ni kubwa kwa Madrid ambao wamekuwa wakimtegemea Rodrygo katika safu ya ushambuliaji msimu huu, Kocha wa timu hiyo sasa atalazimika kupanga upya kikosi chake ili kuziba pengo la mchezaji huyo muhimu.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments