Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Baada ya muda mrefu wa tetesi zikienea zikidai kuwa kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Elie Mpanzu, hana furaha ndani ya klabu hiyo, hatimaye nyota huyo ameweka wazi mustakabali wake kwa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia timu hiyo.
Mpanzu, amesaini kandarasi ya miaka miwili leo Machi 23, 2026, akimaliza uvumi uliokuwa ukihusishwa na uwezekano wa kuondoka kwake ndani ya kikosi hicho chenye maskani yake Dar es Salaam.
Uongozi wa Simba kupitia Rais wa klabu, Mohammed Dewji, umefanikisha mchakato huo muhimu wa kumbakiza nyota huyo, huku ukipata baraka za Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Crescentius Magori.
Hatua hiyo inaonekana kuwa ni ishara ya imani kubwa kwa mchezaji huyo, licha ya kelele za muda mrefu kutoka kwa mashabiki na wachambuzi waliokuwa wakihusisha hali ya kutoridhika kwa Mpanzu ndani ya klabu hiyo.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment